Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2025/2026, Majina 2115

Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2025/2026, Majina 2115 Ajira Immigration

Hii hapa Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2025/2026 Majina 2115. Kuitwa kwenye usaili Immigration Leo, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana walioomba Ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Uhamiaji na waliopokea barua pepe na ujumbe wa simu kufika kwenye usaili kama ifuatavyo:-
Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2025/2026, Majina 2115

Waombaji walioombea Tanzania Bara wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Maktaba (Library) Ndaki ya Elimu (CoED) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tarehe 15 Januari, 2025 saa 1:00 asubuhi. Aidha, waombaji wa Zanzibar wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Hall uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 15 Januari, 2025 saa 1:00 asubuhi.

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na namba ya ombi la Ajira (Application ID) iliyochapishwa kama ilivyotumwa kwenye namba za simu na barua pepe, Kitambulisho chenye picha yake (Mfano, Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Kitambulisho chochote kinachomtambulisha kwa sasa) pamoja na Kalamu ya wino wa bluu.

Kwa waombaji wenye fani za TEHAMA na ufundi magari wajiandae kwa usaili wa vitendo (Practical Examination).

Waombaji walioitwa kwenye usaili wamejulishwa kupitia namba zao za Simu na ujumbe wa barua pepe (e-mail) kama ilivyoainishwa katika Mfumo. Aidha, Wasailiwa wote watatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili.

Aidha, Orodha ya Majina ya waliochaguliwa inapatikana kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji (www.immigration.go.tz).

Pakua PDF hapo chini.
 

Attachments

Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom