SIFA ZA MUOMBAJI AJIRA JESHI LA POLISI TANZANIA

SIFA ZA MUOMBAJI AJIRA JESHI LA POLISI TANZANIA 2025

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Jeshi la Polisi Tanzania linapokea maombi ya ajira kutoka kwa vijana wenye sifa zinazohitajika. Ajira hii inatoa fursa kwa Watanzania wenye nia ya kuhudumu katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
SIFA ZA MUOMBAJI AJIRA.webp


Sifa za Kujiunga na Jeshi la Polisi


Kwa mujibu wa tangazo la Jeshi la Polisi, waombaji wa nafasi hizi wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Uraia
    • Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
    • Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
  2. Elimu na Umri
    • Awe amehitimu kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2019 hadi 2024.
    • Waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri wa miaka 18 hadi 25.
    • Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri wa miaka 18 hadi 30.
  3. Ufaulu wa Masomo
    • Kidato cha nne: Ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne (Division I – IV). Waombaji wenye Division IV wanapaswa kuwa na alama (Points) kati ya 26 hadi 28.
    • Kidato cha sita: Ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu (Division I – III).
  4. Vigezo vya Kimwili
    • Urefu wa angalau futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume.
    • Urefu wa angalau futi tano na inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
  5. Nyaraka Muhimu
    • Awe na kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA.
  6. Uwezo wa Lugha
    • Awe na uwezo mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza.
  7. Afya na Tabia
    • Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
    • Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
    • Asiwe na historia ya uhalifu.
    • Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
  8. Maadili na Utayari wa Kufanya Kazi
    • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
    • Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.
    • Awe tayari kufanya kazi mahali popote Tanzania.
    • Awe hajaajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
    • Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa.

Utaratibu wa Kutuma Maombi


Waombaji wanapaswa kufuata taratibu zifuatazo ili kuhakikisha maombi yao yanapokelewa na kushughulikiwa ipasavyo:

  1. Kuandika Barua ya Maombi
    • Barua ya maombi iandikwe kwa mkono (Handwriting).
    • Ijumuishwe na namba ya simu ya muombaji.
    • Ielekezwe kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kupitia anuani:

      Mkuu wa Jeshi la Polisi
      S.L.P 961
      Dodoma, Tanzania
    • Barua hiyo iambatishwe kwenye mfumo wa maombi ikiwa katika muundo wa PDF.
  2. Kutuma Maombi Kupitia Mfumo wa Mtandaoni
    • Maombi yote yafanywe kupitia mfumo rasmi wa Ajira wa Polisi unaopatikana katika tovuti ya Jeshi la Polisi:
      TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL
    • Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe au kwa mkono hayatapokelewa.

Tarehe ya Mwisho ya Kutuma Maombi


Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kabla ya tarehe 04 Aprili 2025. Kwa maelezo zaidi kuhusu ajira Jeshi la Polisi, tembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi Tanzania.
 
Last edited:
Mimi nilikuwa na swali kwenye hizo ajira za polisi kwa mfano kuna mtu ana four ya 30 na amesomea veta ufundi umeme kamaliza sasa apo vipi
 
Back
Top Bottom