Simba Yaanza Mazoezi Nchini Tunisia Leo 02 January 2025.

Simba Yaanza Mazoezi Nchini Tunisia Leo 02 January 2025.

Revoo

Member

Reputation: 20%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
180
Kikosi cha Simba Sports Club kimefanya mazoezi ya kwanza nchini Tunisia tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika ๐—ง๐—ผ๐˜๐—ฎ๐—น๐—˜๐—ป๐—ฒ๐—ฟ๐—ด๐—ถ๐—ฒ๐˜€๐—–๐—”๐—™๐—–๐—– dhidi ya CS Sfaxien๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ณ utakaopigwa Jumapili Januari 5.

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa nje wa Olympique De R โ€“ Tunis ambao ndio utatumika kwa ajili ya mchezo huo siku ya Jumapili saa moja usiku kwa saa za Tanzania.
FB_IMG_1735853760339.webp

Wachezaji wote 22 waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo kwenye hali nzuri huku wakiendelea kuzoea hali ya hewa.

Akizungumzia hali ya kikosi tangu tulivyowasili Tunisia jana jioni, Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema "kila kitu kinaendelea vizuri na hali ya hewa sio baridi kali na haitakuwa kikwazo siku ya mchezo"

โ€œLeo tumeanza mazoezi kwa siku ya kwanza, tutaendelea kesho pamoja na Jumamosi kabla ya kushuka dimbani Jumapili"

โ€œMaandalizi kwa ujumla yanaendelea vizuri na jambo la kushukuru baridi sio kali kama tulivyoenda Algeria kwahiyo tunaamini tutakuwa na nafasi nzuri ya kupata matokeo chanya,โ€ amesema Ahmed
 
Back
Top Bottom