S

Technical Teachers Registration NACTVET

Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Sura ya 129, kifungu cha 5(1)(b) na marekebisho ya mwaka 2021 kifungu cha 24(1)(a), inalielekeza baraza kusajili walimu wa TVET na mafundi waliobobea. Kwa hiyo, walimu wa TVET na mafundi wanatakiwa kujisajili na kupata NACTVET Registration ID.

Maelekezo Muhimu:
  • Tafuta TRID (Teachers Registration Identification) kutoka kwa Afisa wa Udahili wa taasisi yako.
  • Kabla hujaanza kujisajili, hakikisha tayari umeshahudhuria mafunzo ya mtandaoni ya CBET. Kama bado hujahudhuria, bonyeza eLearning kuanza.
  • Hakikisha una nyaraka zote muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye mwongozo wa usajili. Bonyeza hapa kupakua mwongozo wa usajili.
  • Kama una vyeti vya nje ya nchi, hakikisha vimehakikiwa – kwa wale wa ngazi ya chuo kikuu kupitia TCU, na kwa ngazi ya cheti au diploma kupitia NACTVET.
  • Bonyeza hapa au sehemu ya Registration hapo juu ili kuanza kujisajili.
TVET Teachers' Registration
 
Back
Top Bottom