Tetesi za Usajiri Dirisha Dogo December 2024, Ligi Kuu Tanzania.

Tetesi za Usajiri Dirisha Dogo December 2024, Ligi Kuu Tanzania.

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba inafuatilia kwa karibu kiwango cha Allan Okello (24) mchezaji wa Klabu Vipers inayoshiriki Ligi kuu Nchini Uganda.

Okello, ni miongoni mwa vijana waliojaliwa kipaji kwani huwa anaitwa na kianza kwenye kikosi cha kwanza cha Uganda Cranes licha ya Timu hiyo kuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje ya taifa hilo.

Simba bado hawajatuma ofa kuelekea Vipers lakini wanafurahishwa na kiungo huyo mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto.
FB_IMG_1734367945489.webp

Klabu ya Singida Black stars imeachana na mshambuliaji Joseph guede raia wa Ivory Coast baada ya kufikia makubaliano baina ya pande zote mbili,

Guede ameitumikia Singida katika michezo 6 ya Ligi Kuu ni sawa na dakika 219.

Guede mpaka anachana na Singida Blsck Stats hajafanikiwa kufunga bao lolote tangu ajiunge na klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kuachana na Young Africans mwishoni mwa msimu 2023/24.
FB_IMG_1734434083274.webp

Mshambuliaji Jonathan Sowah atajiunga na Singida Black Stars kwenye hili dirisha dogo la usajili, Sowah anaenda kuchukua nafasi ya Joseph Guede ambae ameachwa Singida Black Stars.

Sowah anaenda kuwa ndiye mchezaji anaelipwa zaidi kwenye kikosi cha Singida Black Stars.
FB_IMG_1734434141210.webp

Singida Black Stars 🇹🇿 imekamilisha usajili wa beki wa kati Frank Assinki (22) raia wa Ghana 🇬🇭 kwa mkataba wa miaka minne akitokea Inter Allies.

Assinki ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Ghana U23 na alikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichobeba AFCON ya U20 mwaka 2021, akiwa na Mshambuliaji Abdul Fatawu anayecheza Leicester City.

Assinki aliwahi pia kupita HB Koge 🇩🇰 akiwa na Victorien Adebayor 🇳🇪.
FB_IMG_1734434193820.webp

Klabu ya Yanga SC ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa ulinzi wa kati Laurian Makame (22) kutoka Fountain Gate

Yanga SC wanapambana kukamilisha dili la beki wa kati Laurian Makame kwa wakati ili kuimarisha kikosi chao.
FB_IMG_1734434282819.webp

Gibril Sillah amepewa ofa rasmi ya USD $125k ili asaini mkataba mpya Azam FC leo.

Sillah ana wiki moja (siku 7) kuamua kama ataendelea au ataondoka klabuni.

Inafahamika kuwa Simba SC na Yanga SC zote zinamtaka Sillah lakini hakuna ofa rasmi kutoka pande zote mbili.

Ni juu ya Sillah kuchukua uamuzi.
FB_IMG_1734434317420.webp

UONGOZI wa Singida Black Stars upo hatua ya mwisho ya kumalizana na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamond ili kuchukua mikoba iliyoachwa na Patrick Aussems ‘Uchebe’.

Uchebe alisimamishwa kazi kwa kuvunjiwa mkataba na Singida baada ya matokeo mabaya mfululizo akianza na kichapo na Yanga bao 1-0 na sare mfululizo dhidi ya Coastal Union na Tabora United na kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Ramadhan Nsanzurwimo na David Ouma.

Habari zilizonaswa na Wananchiforum ni kwamba Singida ipo katika hatua nzuri ya mazungumzo kumalizana na Gamondi aliyeondolewa Yanga akiwa ameweka rekodi mbalimbali katika Ligi Kuu na michuano ya CAF kwa klabu hiyo kongwe.

Chanzo cha kuaminika kutoka Singida, kimeambia Wananchiforum kuwa, mazungumzo na kocha huyo yapo pazuri na wale waliopo sasa watakuwa wasaidizi wa Gamondi mwenye uraia wa Argentina.

“Tunatambua ubora wa mbinu na CV kubwa ya Gamondi itakuja kuongeza thamani ya timu na kukuza vipaji vya wachezaji wetu ambao malengo yao makubwa ni kuipambania timu yetu kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Tuna matarajio makubwa kumpata kabla ya dirisha la usajili kufungwa ili apate nafasi ya kupendekeza usajili katika dirisha dogo la usajili lililofunguliwa Desemba 15, 2024 na linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2025.”

Gamondi aliondolewa Yanga baada ya vipigo viwili mfululizo akianza na Azam FC 1-0, na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Tabora United zote zikichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex.
images-32-20.webp

Mshambuliaji Fahad Bayo raia wa Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya Yanga SC akiwa ni mchezaji huru. Bayo mwenye umri wa miaka 26 anachukua nafasi ya mshambuliaji Jean Baleke ambaye atatolewa kwa mkopo Namungo FC.
FB_IMG_1734434475077.webp
 

Attachments

  • FB_IMG_1734434408898.webp
    FB_IMG_1734434408898.webp
    41.1 KB · Views: 35
Back
Top Bottom