Uchambuzi Mechi Ya Leo Jumamosi 28 December 2024: Singida black star 0 vs 1 Simba sports club.

Uchambuzi Mechi Ya Leo Jumamosi 28 December 2024: Singida black star 0 vs 1 Simba sports club.

Revoo

Member

Reputation: 18%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
160
Simba na 4-2-3-1 , waliamua kufanya mabadiliko kwenye eneo la kiungo (Kagoma na Ngoma) wakianza kama “Double Pivot” then Ahoua mbele yao huku Mpanzu na Kibu wakitokea pembeni …. Nini Simba walikifanya wakiwa na mpira ?

✍️ Build Up yao ilikuwa nzuri na 2-4 (CBs wawili + viungo wawili wa chini then Zimbwe na Kapombe wanakuwa mstari mmoja na viungo hao) Hamza na Malone walipata “Option” nyingi za kupasia mipira , kwasababu Singida hawakuwa na namba nzuri ya wachezaji wakati wanapress … How ?

✍️ Ngoma na Kagoma mmoja alikuwa free bila presha yeyote (Rupia Vs Hamza na Malone then Anthur Vs Ngoma & Kagoma huku Tchekei na Keyekeh Vs FBs wa Simba , hapo ni 6 Vs 4 ) ngumu kwa Singida kuizuia “Build Up” ya Simba na Fadlu alileng’a zaidi kushambulia kwa kutumia mawings wake (Mpanzu na Kibu) wacheze wakiwa pembeni zaidi .

✍️ Zimbwe na Kapombe mda mwingi hawakusogea juu sana dhumuni ni kulinda nafasi nyuma yao hivyo Mpanzu na Kibu mda mwingi walishambulia eneo la pembeni ya uwanja na kuwafanya Singida kuzuia eneo kubwa la uwanja (kuwatanua walinzi wa Singida) nafasi zikaanza kufunguka katikati ya uwanja + Simba walipora mipira mingi wakati Singida wanaanza “Build Up” yao , hapo Simba walipata nafasi kubwa kwenye mpira na space zilifunguka kwa mawings wao .

Singida walipoteza pasi kirahisi hasa wanapoanza “Build Up” walikutana na pressing bora kutoka kwa Simba + idadi ya wachezaji ilikuwa ndogo . Nafikiri Singida mtego wao ulikuwa kushambulia kwa “Counter Attacks” pale wanapopora mipira wanashambulia kwa haraka sana lakini pasi zao za mwisho zilikosa ubora .
FB_IMG_1735400287775.webp


NOTE :

Kagoma amevuruga plan nyingi za Singida Black Stars 👏 Ngoma”Classy” amecheza game bora sana .

Anthur Bada “What a player ✅” ametoa game bora kwa Simba : Pass. , Componsure 🙌 mali mguuni kwake ukichukua Faul .

Metcha Mnata 🤔 Kafanya kosa la kitoto sana …. Yule Camara 🔥

Jean Ahoua : Assist 5 mpaka sasa NBCPL .

FT : Singida Black Stars 0-1 Simba .
FB_IMG_1735397887093.webp
 
Back
Top Bottom