What's new

waliodahiliwa zaidi ya Chuo Kimoja au Programu zaidi ya moja katika awamu ya Tatu 2024/2025

Sia

Member
waliodahiliwa zaidi ya Chuo Kimoja au Programu zaidi ya moja katika awamu ya Tatu 2024/2025

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimuya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa udahili katikaAwamu ya Tatu na ya mwisho kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katikaTaasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2024/2025umekamilika. Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yanatangazwana vyuo husika.
Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Tatu na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita, wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 19 hadi 21 Oktoba, 2024. Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).

Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.
Bonyeza hapa kudownload majina yote
 
Back
Top