- Joined
- Dec 12, 2024
- Messages
- 169
Wawili Simba Kuikosa Singida Black Stars Leo
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa Kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Black Stars ambao utapigwa Leo Jumamosi katika uwanja wa CCM LITI.
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari jana, Fadlu amesema kwamba licha ya kukabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo, wamejiandaa vyema na mchezo huo, malengo ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
“Tumejipanga kukabiliana na timu nzuri, Leo (Jana) tutakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi yetu ya mwisho tukiwa na wachezaji wote baada ya kufanya recovery kwa siku mbili kuondoa uchovu kwa wachezaji waliotumika zaidi. Tumecheza mechi nne katika kipindi cha siku nane”
“Tunajua ubora wao, wanaweza kufunga mabao kuanzia eneo lao la kiungo na safu ya ushambuliaji lakini sisi hatutakwenda kucheza kwa lengo la kuwazuia bali kuhakikisha tunatawala mchezo na kutumia vyema nafasi tutakazotengeneza”
“Naamini njia sahihi ya kuzuia ni kumiliki mchezo na kuwabana wapinzani katika eneo lao, kwa kufanya hivyo tunajitengenezea mazingira mazuri ya kufunga na kuwanyima nafasi ya kutudhuru,” alisema Fadlu
Aidha Fadlu amesema kuwa katika mchezo huo Simba itawakosa wachezaji wawili ambao ni Joshua Mutale kutokana na majeraha na Valentine Nouma aliyesafiri kwenda nyumbani Burkina Faso kwaajili ya kufunga ndoa.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Mshambuliaji Awesu Awesu amesema kuwa wanatarajia mchezo huo utakuwa mgumu hasa ikizingatiwa wanakwenda kucheza dhidi ya timu yenye wachezaji wengi wenye uzoefu lakini watapambana ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
“Mechi itakuwa ngumu kulingana na wachezaji wa wapinzani wetu wengi ni wazuri na wana uzoefu ila tumejipanga vizuri dhidi yao kuhakikisha tunapambania pointi tatu katika mechi hii,” alisema Awesu