Wengine Hawapo Kwenye Mipango Ya Mchezo Simba Sports Club Dhidi Ya Bravo Do Maquis TotalEnergies CAFCC

Wengine Hawapo Kwenye Mipango Ya Mchezo Simba Sports Club Dhidi Ya Bravo Do Maquis TotalEnergies CAFCC 2024/2025

Revoo

Member

Reputation: 21%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
190
Simba SC itacheza dhidi ya Bravos FC ya Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la CAF Jumapili, Januari 12, 2025, lakini wachezaji wanne muhimu wameachwa nyuma. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Steven Mukwala, Valentine Nouma na Joshua Mutale.
FB_IMG_1736268760382.webp

Katika orodha ya wachezaji 22 waliosafiri na timu, Mutale anasumbuliwa na majeraha, lakini wachezaji wengine wameachwa kwa kuzingatia mahitaji ya kimkakati ya mchezo huo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ali, alithibitisha kwamba kocha Fadlu Davids ameendelea na utaratibu wake wa kufanya mabadiliko katika kikosi (rotation), kulingana na changamoto za kila mchezo.

“Kocha ameangalia mahitaji ya mchezo dhidi ya Bravos FC na kufanya mabadiliko ya kawaida ya kikosi chake. Hivyo basi, wachezaji hawa wameachwa nyuma kwa sababu ya mahitaji maalum ya mchezo,” alisema Ahmed Ali.

Manula, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na timu, ameendelea kuachwa nje ya kikosi licha ya juhudi zake za kurejea uwanjani. Taarifa zinasema kuwa, kwa mujibu wa dirisha la usajili, huenda Manula akaondoka Simba kwa mkopo kabla ya dirisha hili kufungwa.

“Hakuna tatizo lolote kwa wachezaji hawa kubaki. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa wa kocha,” aliongeza Ahmed Ali.

Simba itaendelea na maandalizi ya mchezo huo muhimu huku ikitumaini kurejea na matokeo mazuri kutoka Angola.
 
Back
Top Bottom