Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Novemba 2024, zitakazotumika kuanzia tarehe 6 Novemba saa 6:01 usiku. Bei za mafuta ya petroli, dizeli, na mafuta ya taa zimepanda kutokana na mabadiliko ya bei za soko la kimataifa. Wafanyabiashara wanatakiwa kuuza kwa bei zilizowekwa na EWURA ili kuepuka hatua za kisheria.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za bidhaa za mafuta nchini Tanzania, zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia Jumatano, 6 Novemba 2024 saa 6:01 usiku. Bei hizi za mafuta ya petroli, dizeli, na mafuta ya taa zimepangwa kwa mujibu wa mwenendo wa bei za soko la kimataifa na gharama za uagizaji katika bandari za Dar es Salaam, Tanga, na Mtwara.
Kwa mwezi Novemba, EWURA imeainisha bei za rejareja na za jumla kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, na Mtwara kama ifuatavyo:
Soma zaidi: Matokeo ya uchaguzi Marekani

Bei Kikomo za Mafuta Novemba 2024
Kwa mwezi Novemba, EWURA imeainisha bei za rejareja na za jumla kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, na Mtwara kama ifuatavyo:
Jedwali la Bei:
- Jedwali Na. 1: Bei za Rejareja kwa Mikoa Mbalimbali
- Jedwali Na. 2: Bei za Jumla kwa Wafanyabiashara
Mwenendo wa Bei na Sababu za Mabadiliko
- Bei kikomo za mafuta kwa mwezi Novemba 2024 zimepangwa kwa kuzingatia bei za mafuta safi (FOB) kutoka soko la kimataifa la Uarabuni kwa mwezi Oktoba 2024.
- Ikilinganishwa na mwezi uliopita wa Septemba 2024:
- Bei ya mafuta ya petroli imeongezeka kwa asilimia 1.56%
- Bei ya dizeli imepanda kwa asilimia 4.99%
- Bei ya mafuta ya taa imeongezeka kwa asilimia 4.74%
Gharama za Uagizaji (Premiums) na Ubadilishaji Fedha
Kwa mujibu wa EWURA:- Gharama za uagizaji (Premiums) za petroli zimepungua kwa wastani wa 3.91% katika Bandari ya Dar es Salaam, huku gharama za dizeli zikipanda kwa 14.48%.
- Hakuna mabadiliko kwa gharama za mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam.
- Katika bandari ya Mtwara, gharama zimepanda kidogo kwa wastani wa 0.67%.
Soma zaidi: Matokeo ya uchaguzi Marekani