What's new
Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal | Mwongozo wa Kufungua Account Ajiraportal

PDF Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal | Mwongozo wa Kufungua Account Ajiraportal 2024

Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal | Mwongozo wa Kufungua Account Ajiraportal. Mwombaji kazi anapaswa kuingiza namba yake sahihi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwenye mfumo. Baada ya kuingiza namba hiyo, mfumo utamuuliza maswali ya uthibitisho ili kuhakikisha kuwa namba ni sahihi na inahusiana na mwombaji. Taarifa zikithibitishwa, mfumo utachukua taarifa kutoka NIDA na kuziingiza moja kwa moja kwenye mfumo wa maombi ya kazi.
Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal


Baada ya taarifa zake kuingizwa, mwombaji kazi anatakiwa kukamilisha kuingiza taarifa nyingine muhimu za kibinafsi na kubonyeza kitufe cha "Hifadhi" ili taarifa ziweze kuhifadhiwa kwa uhakika kwenye mfumo wa ajira.

Link za Ajira Portal

  1. Matangazo ya Kazi
    Link: https://portal.ajira.go.tz/advert/index
    Hii ni sehemu yenye matangazo ya kazi, ambapo waombaji wanaweza kuona kazi zote zilizotangazwa kwenye Ajira Portal.
  2. Kuingia kwenye Akaunti
    Link: https://portal.ajira.go.tz/user/auth/login
    Hii ni link ya kuingia kwa watumiaji waliosajiliwa tayari.
  3. Kujisajili kwa Akaunti Mpya
    Link: https://portal.ajira.go.tz/user/auth/registration_user
    Hii ni kwa waombaji wapya wanaotaka kujiandikisha kwenye Ajira Portal.
  4. Maoni na Mrejesho
    Link: https://portal.ajira.go.tz/feedback
    Hii ni sehemu ya kutoa maoni na mrejesho kuhusu uzoefu na huduma zinazotolewa kwenye Ajira Portal.

Makundi ya Nafasi za Kazi Zinazopatikana​

  1. Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu - Nafasi 2
  2. Benki, Uchumi na Huduma za Fedha - Nafasi 3
  3. Sayansi Asilia na Mazingira - Nafasi 2
  4. Ubunifu na Sanaa za Kuunda - Nafasi 8
  5. Elimu na Mafunzo - Nafasi 15
  6. Uhandisi na Ujenzi - Nafasi 40
  7. Sayansi ya Mazingira na Jiografia - Nafasi 5
  8. Ufugaji na Kilimo - Nafasi 5
  9. Huduma za Afya na Dawa - Nafasi 15
  10. Rasilimali Watu na Utawala - Nafasi 13
  11. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - Nafasi 13
  12. Sheria - Nafasi 2
  13. Lugha - Nafasi 4
  14. Masoko, Vyombo vya Habari na Bidhaa - Nafasi 3
  15. Usimamizi wa Miradi, Mipango na Sera - Nafasi 1
  16. Utafiti, Sayansi na Bioteknolojia - Nafasi 4
  17. Sosholojia, Sayansi ya Siasa, Maendeleo ya Jamii - Nafasi 7
  18. Utalii na Usafiri - Nafasi 7
  19. Usafirishaji na Usafiri - Nafasi 6
  20. Usimamizi wa Ardhi - Nafasi 8
  21. Maji, Madini na Rasilimali Asilia - Nafasi 3
  22. Kilimo na Rasilimali Asilia - Nafasi 1
Kwa kutumia link hizi na kuangalia makundi ya kazi, waombaji wanaweza kufuatilia nafasi zinazolingana na taaluma zao na kuomba moja kwa moja kupitia mfumo wa Ajira Portal.

Mwombaji kazi pia anatakiwa kuingiza taarifa za mawasiliano, ikiwemo sanduku la posta, namba ya simu, barua pepe, na anuani ya makazi (kuanzia nchi, mkoa, hadi wilaya). Majibu mengine yatachaguliwa kutoka kwenye orodha ya mfumo, lakini namba ya simu lazima iingizwe kwa mkono.

Kuhusu taarifa za elimu, mwombaji kazi anapaswa kuchagua kiwango chake cha elimu kwenye sehemu ya "Educational Level." Inashauriwa aanze na kuingiza taarifa za kidato cha nne na kuendelea kulingana na kiwango chake cha elimu. Kwa elimu ya juu zaidi, mwombaji anatakiwa kuchagua kundi la kozi (Programme Category). Ikiwa kozi haipo kwenye kundi alilochagua, itambue kuwa kundi halijachaguliwa vizuri na anapaswa kurudi na kuchagua upya. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania, wanatakiwa kuchagua kundi linaloendana na kozi yao, na Sekretarieti ya Ajira itakagua usahihi wa taarifa hizo.
Ajira Recruitment Portal


Chagua fani uliyofuzu na inatakiwa jina lake lifanane na kilichoandikwa kwenye cheti chako cha kuhitimu ambacho unataka kukiambatisha kwenye mfumo, endapo hujapata jina linaloendana na kozi uliyomaliza huenda umechagua sehemu isiyo sahihi na taaluma yako, hivyo tafuta sehemu nyingine kwa kutumia jina la fani uliyofuzu kama ilivyoandikwa kwenye cheti chako.
Program category ajira portal
Author
Gift
Downloads
256
Views
1,087
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Back
Top