Jinsi ya Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma 2024/2025 | Utumishi au TAMISEMI

PDF Jinsi ya Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma 2024/2025 | Utumishi au TAMISEMI 20241109

Hatua Muhimu za au jinsi ya Kuomba Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi | Watumishi wa Umma 2024/2025 Kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwenda TAMISEMI.

Kwa mtumishi anayehitaji kuhamishwa kwenda sehemu nyingine kupitia TAMISEMI, ni muhimu kuwa na nyaraka zote zinazohitajika ili kuharakisha mchakato wa kuidhinisha uhamisho wake. Hapa ni mwongozo wa nyaraka na maelezo yanayohitajika:
  1. Barua ya Maombi ya Kibali cha Uhamisho kutoka kwa Mwajiri (Mkurugenzi): Mwajiri wa mtumishi, ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri au idara husika, anatakiwa kuandika barua rasmi ya kumuombea mtumishi kibali cha uhamisho.
  2. Barua ya Maombi ya Uhamisho ya Mtumishi: Mtumishi lazima awe ameshaandika barua ya maombi ya uhamisho na kuituma kwa mwajiri wa mahali anakotaka kuhamia. Barua hii inaonesha nia ya mtumishi na ni hatua muhimu katika mchakato.
  3. Barua ya Kukubaliwa Uhamisho kutoka kwa Mwajiri Mpya: Barua hii ni uthibitisho kuwa mwajiri wa mahali anakotaka kuhamia ameridhia maombi ya mtumishi kuhamia huko. Ni nyaraka muhimu kuonyesha kuwa nafasi hiyo ipo na mwajiri yuko tayari kumpokea mtumishi.
  4. Barua ya Ajira: Mtumishi anapaswa kuwa na nakala ya barua yake ya kuajiriwa, inayoonesha rasmi kuwa yuko kazini na mwajiri wake wa sasa.
  5. Barua ya Kuthibitishwa Kazini: Hii ni nyaraka inayoonesha kwamba mtumishi amethibitishwa kazini baada ya kipindi cha majaribio na ameidhinishwa kuendelea na ajira hiyo.
  6. Kitambulisho cha Kazi: Nakala ya kitambulisho cha kazi cha mtumishi inahitajika kama sehemu ya uthibitisho wa utambulisho wake na cheo alichonacho.
  7. Hati ya Mshahara (Salary Slip): Mtumishi anatakiwa kuwasilisha nakala ya hati yake ya mshahara ya hivi karibuni ili kuthibitisha mshahara anaopokea na mahali pa kazi.
  8. Kiambatisho cha Sababu za Uhamisho: Mtumishi anatakiwa kuwa na kiambatisho kinachoelezea sababu za uhamisho wake. Hii inaweza kuwa na vielelezo maalum kutegemea sababu zifuatazo:
    • Kumfuata Mwenza: Ikiwa mtumishi anaomba uhamisho ili kumfuata mwenza, anatakiwa kuwasilisha cheti cha ndoa kama uthibitisho.
    • Sababu za Kifamilia: Kama uhamisho unahitajika kwa sababu za kifamilia (kama vile kuwahudumia wazazi au ndugu wanaomtegemea), mtumishi anapaswa kuwa na barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata, Kijiji, au Mtaa wa sehemu anakokwenda.
    • Sababu za Kiafya: Ikiwa mtumishi anahitaji kuhama kwa ajili ya matibabu, barua ya rufaa au ripoti kutoka kwa daktari wa hospitali ya serikali inapaswa kuambatanishwa. Barua hiyo inatakiwa kuonesha kuwa mtumishi anahitaji kupata matibabu katika hospitali iliyopo karibu na eneo analotaka kuhamia.
    • Kubadilishana Nafasi na Mtumishi Mwenzake: Kama mtumishi anabadilishana na mtumishi mwenzake, taarifa zote za mtumishi wanayebadilishana naye zinapaswa kuambatanishwa.
Jinsi ya Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma 2024/2025 | Utumishi au TAMISEMI

Kuzingatia na kukamilisha nyaraka hizi ni hatua muhimu kwa mtumishi anayehitaji uhamisho kupitia TAMISEMI, kwani itaharakisha na kuondoa changamoto katika mchakato wa kupata kibali.
Soma zaidi: Jinsi ya kuhama kituo kwa watumishi wa Umma 2024
Author
GiftVerified member
Downloads
199
Views
541
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Similar resources Most view View more
Back
Top Bottom