Mabadiliko ya Sehemu ya kufanyia Usaili TRC Utumishi | Shirika la Reli Tanzania

Ajira Mabadiliko ya Sehemu ya kufanyia Usaili TRC Utumishi | Shirika la Reli Tanzania 31 Oktoba 2024

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Kama wewe ni miongoni mwa wasailiwa wa kada ya Mechanical Artisans II (Shirika la Reli Tanzania - TRC), tunayo habari muhimu kuhusu mabadiliko ya mahali pa kufanyia usaili wa mahojiano.
Mabadiliko ya Sehemu ya kufanyia Usaili TRC Utumishi | Shirika la Reli Tanzania

Mabadiliko ya Mahali:
Usaili wa mahojiano sasa utafanyika katika Ofisi za Shirika la Reli Tanzania (TRC) Makao Makuu, Dar es Salaam, badala ya Ofisi za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kama ilivyooneshwa kwenye tangazo la awali la kuitwa kwenye usaili la tarehe 25.10.2024, lenye kumbukumbu Na. JA.9/259/01/B/92.

Tarehe na Muda:
Tarehe na muda wa usaili utabaki kama ulivyo kwenye tangazo la awali, hivyo tunakuhimiza uhakikishe unajiandaa ipasavyo.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia:

  1. Pata Taarifa Zote: Kwa taarifa zaidi na maelezo ya kina, tembelea tovuti yetu www.ajira.go.tz ili kuhakikisha unapata habari sahihi na za hivi punde.
  2. Jipange Vizuri: Tumia muda huu kujihakikishia kuwa uko tayari kwa mahojiano. Fanya mazoezi ya maswali yanayoweza kuulizwa na kujiandaa vizuri.
  3. Ufuatiliaji: Kuwa makini na tangazo lolote la ziada ambalo linaweza kutolewa kuhusu usaili ili usikose taarifa muhimu.
Tunawatakia kila la kheri katika usaili wenu. Hakikisha unafika kwa wakati na uweze kuonyesha ujuzi wako vyema!
Soma zaidi: Mabadiliko ya usaili IFM

Kuhusu TRC: Shirika la Reli Tanzania (TRC) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017. Lengo kuu la TRC ni kutoa huduma za usafiri wa reli na kuendeleza, kukuza, na kusimamia miundombinu ya reli.
Author
GiftVerified member
Downloads
99
Views
275
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Similar resources Most view View more
Back
Top Bottom