What's new
Matokeo ya Darasa la Saba 2024 NECTA PSLE Yametoka Rasmi Leo | Jinsi ya Kuangalia www.necta.go.tz

NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2024 NECTA PSLE Yametoka Rasmi Leo | Jinsi ya Kuangalia www.necta.go.tz 29 Oktoba 2024

Matokeo ya Darasa la Saba Yatangazwa na Baraza la Mitihani
Katika kutangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi jijini Dar es Salaam jana, Oktoba 29, 2024, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Dkt. Said Mohamed, ametoa takwimu za jumla za watahiniwa waliosajiliwa na walioshiriki katika mtihani huu muhimu.
Kulingana na taarifa hiyo, jumla ya watahiniwa 1,230,774 walisajiliwa kufanya mtihani, wakiwemo wasichana 666,597 (sawa na asilimia 54.16%) na wavulana 564,177 (sawa na asilimia 45.84%). Kati ya hawa, 4,583 walikuwa watahiniwa wenye mahitaji maalum, wakichangia asilimia 0.37 ya watahiniwa wote.
Aidha, watahiniwa 1,204,899 (sawa na asilimia 97.90%) walihudhuria na kufanya mtihani huu. Kati ya walioshiriki, 656,160 walikuwa wasichana (asilimia 98.43) na 548,739 walikuwa wavulana (asilimia 97.26).

Muhtasari wa Takwimu za Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2024​

KipengeleIdadi ya WatahiniwaAsilimia
Watahiniwa Waliosajiliwa1,230,774100%
- Wasichana666,59754.16%
- Wavulana564,17745.84%
Watahiniwa Wenye Mahitaji Maalum4,5830.37%
Watahiniwa Waliofanya Mtihani1,204,89997.90%
- Wasichana656,16098.43%
- Wavulana548,73997.26%
Baraza linawapongeza watahiniwa wote walioshiriki na linatoa shukrani kwa wale wote waliohusika kuhakikisha mtihani huu unafanyika kwa ufanisi.
  • Like
Reactions: Edina
Back
Top