Mwongozo wa Kuomba Ufadhili wa Commonwealth Scholarship Tanzania 2025-2026. Commonwealth scholarships ni scholarships ambazo hutolewa na Kamisheni ya Ufadhili yaCommonwealth (Commonwealth Scholarship Commission-CSC) iliyopo nchini Uingerezakupitia ofisi ya Maendeleo, Mambo ya nje na Jumuiya ya Madola (UK Foreign,Commonwealth and Development Office-FCDO). Ufadhili huu ulianza rasmi mwaka 1960na mpaka sasa wanufaika Zaidi ya 31,000 kutoka nchi mbalimbali wamenufaika na ufadhilihuu. Lengo kuu la fadhili hizi ni kuwasaidia raia hodari kutoka nchi za Jumuiya ya Madolakuweza kusoma katika vyuo vya Uingereza na kuweza kuleta mabadiliko na athari zamaeneleo endelevu hasa katika nchi zao.