What's new
Utaratibu wa Uhamisho wa Watumishi wa Umma 2024/2025 | Kuhama kufata Wenza Utumishi

PDF Utaratibu wa Uhamisho wa Watumishi wa Umma 2024/2025 | Kuhama kufata Wenza Utumishi 20241109

Hizi hapa fomu za maombi ya Utaratibu wa Uhamisho wa Watumishi wa Umma 2024/2025 | Kuhama kufata Wenza Utumishi, Jinsi ya kubadili kituo kimoja kwenda kingine TAMISEMI PDF ipo juu.

Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma zinaeleza jinsi watumishi wa umma wanavyoweza kuhamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwingine. Hii ni kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira ya mwaka 2008, Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298, pamoja na Kanuni za mwaka 2022 na 2009. Utaratibu huu unafanywa ili kuhakikisha watumishi wanatumiwa ipasavyo na kuongeza ufanisi katika shughuli za Serikali.

Mamlaka ya Katibu Mkuu (Utumishi) Kuhusu Uhamisho

Utaratibu wa Uhamisho wa Watumishi wa Umma 2024/2025 | Kuhama kufata Wenza Utumishi

Katibu Mkuu (UTUMISHI) amepewa mamlaka ya kusimamia uhamisho wa watumishi, kwa kuzingatia mahitaji ya Serikali na rasilimali zilizopo. Hii ina maana kuwa Katibu Mkuu anaweza kuidhinisha uhamisho iwapo kuna sababu maalum za kimaslahi kwa Umma.

Uhamisho kwa Sababu ya Kuwafuata Wenza wa Ndoa

Mbali na uhamisho kwa maslahi ya Umma, watumishi pia wanaweza kuomba kuhamishwa kwa sababu ya kuungana na wenza wao wa ndoa. Waraka uliotolewa tarehe 31 Machi, 2006 (Kumb. Na. EA. 45/257/01/49) unaruhusu uhamisho wa aina hii. Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la maombi kutoka kwa watumishi wanaotaka kuhama kwa lengo la kuwafuata wenza wao.

Ili kuwezesha Ofisi ya Katibu Mkuu kuwa na takwimu sahihi, watumishi wanaotaka kuhama kwa sababu hii wanapaswa kuwasilisha taarifa zao kabla au ifikapo tarehe 5 Oktoba, 2024.

Namna ya Kuwasilisha Maombi ya Uhamisho

Watumishi wanaotaka kuhama kwa sababu ya kuungana na wenza wao wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kwa njia zifuatazo:
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
  • Bi. Felister E. Shuli
  • Simu: 0717414688
Author
Gift
Downloads
161
Views
325
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Back
Top