Benki Kuu ya Tanzania (BOT): Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuondoa Kwenye Mzunguko Noti Za Zamani Za Shilingi Ya Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania (BOT): Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuondoa Kwenye Mzunguko Noti Za Zamani Za Shilingi Ya Tanzania

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 100%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
1,651
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuhusu zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoaainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT): Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuondoa Kwenye Mzunguko Noti Za Zamani Za Shilingi Ya Tanzania


Zoezi la ubadilishaji linaratajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa. Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili, 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia katika kufanya malipo popote duniani; na benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Hivyo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani, kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.

Kwa taarifa/msaada zaidi tafadhali wasiliana na: Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939 Dar es Salaam; au kwa Barua Pepe: [email protected] au [email protected]; au kwa simu +255745 802 007.

Soma zaidi: Nafasi za Kazi NMB Bank Octoba 2024
 
Back
Top Bottom