Upimaji wa fani za elimu ya amali utafanyika kwa kuzingatia miongozo ya mitihani, taratibu na miongozo ya utahini na utunuku ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Wanafunzi wote wa Mkondo wa Elimu ya Amali watafanya mitihani ya NACTVET wakiwa Kidato cha II (NVA ngazi ya 1), Kidato cha III (NVA ngazi ya 2) na Kidato cha IV (NVA ngazi ya 3).
Zifuatazo ni Fani Kuu za Mkondo wa Elimu ya Amali
Zifuatazo ni Fani Kuu za Mkondo wa Elimu ya Amali
- Uandisi wa Umeme (Electrical Engineering)
- Uhandisi Mitambo (Mechanical Engineering)
- Uhandisi Ujenzi (Civil Engineering)
- Uhandisi Magari (Automotive Engineering)
- Elektroniki na Kompyuta (Electronics and Computer)
- Huduma za Usafirishaji (Transport and Logistics)
- Ushoni (Clothing and Textile)
- Kilimo, Ufugaji na Usindikaji Vyakula (Agriculture and Food Processing)
- Ukarimu na Utalii (Hospitality and Tourism)
- Huduma Saidizi za Biashara (Commercial and Business Support Services)
- Uchapishaji (Printing)
- Uchimbaji na Uchenjuaji Madini (Minerals Extraction and Processing)
- Urembo na Ususi (Cosmetology)
- Sanaa na Ubunifu (Creative Arts)
- Michezo (Sports)