Hesabu Za Simba Sports Club Kwenye Makundi TotalEnergies CAFCC

Hesabu Za Simba Sports Club Kwenye Makundi TotalEnergies CAFCC 2024/2025

Revoo

Member

Reputation: 22%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
192
Endapo Simba atamaliza Nafasi ya kwanza kwenye kundi lake basi ana nafasi kubwa sana ya Kufika hadi hatua ya Nusu Fainal.
FB_IMG_1736135185977.webp


Endapo simba atamaliza Nafasi ya kwanza basi upo uwezekano mkubwa sana wa kukutana na timu zifuatazo amabzo zinanafasi kubwa ya kumaliza nafasi ya pili kwenye makundi yao.

1. Stellenbosch Fc (South Africa).
2. Asec Mimosas (Ivory coast).
3. Al Masry SC (Egypt)

Moja ya Faida kubwa ni kuanzia ugenini na kumalizia kwa Benjamin mkapa ambayo kimahesabu ina faida kubwa sana.

Simba Sc endapo wakimaliza nafasi ya pili kwenye kundi kuna hati hati ya kukutana na timu zifuatazo ambazo zinanafasi kubwa ya kumaliza kama vinara kwenye makundi yao.

Rs Berkane(Moroco)
USM Alger(Algeria)
Zamalek(Misri)

Vitu viwili kuzihusu hizi timu mbili.

1. Timu zote hizi tatu ni Recent champions wa Kombe la shirikisho kwenye misimu mitatu iliyopita.

Rs Berkane walikua champions 2021/22, USM Alger walikua champions 2022/23 na Zamalek walikua champions msimu uliopita 2023/24.

2. Timu hizi zote zinatoka ukanda mgumu sana kupata matokeo ambapo Simba tangu arejee kwenye ubora wake kwenye michuano ya CAF amepasuka mara zote isipokua jana.

Ikumbukwe pia Kama simba atamaliza nafasi ya pili kwenye kundi ataanzia nyumbani kisha kumalizia ugenini.

Nazani njia pekee ya Simba kupenya hatua ya Robo na kuingia Nusu Fainal ni kuikwepa hii miamba mitatu kwa kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi nje na hapo jina MWAKAROBO litaendelea kutuandama.
 
Back
Top Bottom