- Joined
- Dec 12, 2024
- Messages
- 169
CS Sfaxien wako nyumbani leo kwenye kampeni yao kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na wanacheza dimbani kucheza na Simba Sc.
Sfaxien hawajashinda mchezo wowote katika michezo mitatu waliyocheza na wako mkiani wakiwa hawana alama yoyote mpaka sasa huku wakiwa wameruhusu mabao 6 kwenye wavu wao na wao kufunga mabao matatu.
Kwenye ligi yao wapo nafasi ya 9 wakiwa na alama 17 kwenye michezo 13 waliyocheza hivi karibuni, wameshinda mechi 4, wametoa sare mechi 5 na kufungwa mechi 4.
Kwenye mechi 5 za hivi karibuni wamepoteza zote...
Wanakutana na Simba ambao wana alama 6 kwenye msimamo wa kundi A wakiwa sawa na Bravos na Cs Constantine kwa kila kitu.
Simba wameshinda mechi mbili za nyumbani na kufungwa mechi moja ya ugenini huku wakiwa wamefunga jumla ya mabao manne na kufungwa mabao matatu.
Kwenye Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 40 kwenye mechi 15 na wameshinda mechi 13,wamepoteza moja na kutoa sare mchezo mmoja...
Simba pia wamefunga jumla ya mabao 31 na kuruhusu mabao matano tu.
Kwenye mchezo wa leo Sfaxien wanaingia wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Cs Constantine, walifungwa 1-0 lakini pia Simba akiwa ugenini alifungwa na Cs Constantine mabao 2-1.
Nini maana yake...?
Yoyote anaweza kupata matokeo kwenye mchezo wa leo!
Simba hana rekodi nzuri ugenini na wanakutana na Sfaxien ambao wao pia hawana rekodi nzuri nyumbani pia.
Mwisho, Kama kuna kitu kizuri Simba wanapaswa kuwa nacho leo ni kuhakikisha wanapata alama leo...
Atakaepata alama dhidi ya Sfaxien ndiye atakuwa na uwezo mkubwa wa kusonga mbele kwakuwa kila mtu anashinda kwake.