KUITWA KAZINI KADA ZA AFYA NA TAASISI MBALIMBALI 5 DESEMBA 2024

KUITWA KAZINI KADA ZA AFYA NA TAASISI MBALIMBALI 5 DESEMBA 2024

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 42%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
355
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 03-09-2024 na tarehe 11-09-2024 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili yatatolewa hivi karibuni. Orodha ya wagombea waliofaulu, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wagombea waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili. Baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayatokea katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
KUITWA KAZINI KADA ZA AFYA NA TAASISI MBALIMBALI 5 DESEMBA 2024
 

Attachments

Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
Back
Top Bottom