Naomba tujadili hili swala jamani, je Kuwepo kwa Usaili Kada za Ualimu 2024 Utumishi kutasaidia kupata walimu bora?
View attachment 150
Binafsi yangu naomba nijibu hili suala kwa kutumia hoja za mjadala yakinifu;
1.NDIO, KWA SABABU ZIFUATAZO;
A. Kuondoa mianya ya kupata watumishi wasio na weredi(incompetent personnel).
Kwani watashindwa katika hatua za mchujo kwa kutokuwa na umahiri wa kada na taaluma ya ufundishaji.
B. Lengo la dhana ya umahiri(Competence)katika ngazi ya taifa hususani katika kada ya ualimu litafikiwa. Kwani nyenzo atakazopimwa nazo msahiliwa katika mchujo ndizo zitakazotumika katika upimaji wa mwisho kwa wanafunzi(Final evaluation) hivo kutakuwa na uwiano wa zao(product) na zao lingano(ouput).
C. Usaili utafuta Matumizi ya tarakalishi katika chaguzi za watumishi(Computer Intelligence Command) bali usaili utajikita kuandaa walsahiliwa Bora wa kada ya ualimu.
2. HAPANA, KWA SABABU ZIFUATAZO;
A. Kulingana na muundo wa usaili Kuna hojaji ya maandishi na hojaji ya mazungumzo(oral and written interview) ambapo hujikita kwa kupima katika ngazi ya utambuzi(cognitive domain) na kuacha ngazi zingine muhimu ambazo Mwalimu anabidi apimwe. Hivo Kuna hatari ya kupata wasahiliwa bandia ambao wamepimwa kwa ngazi Moja.
B. Usaili huu kulingana na muundo wake una hatari dhana ya kubahatisha(lucky/intuition) ambapo kwa written interview kama kutakuwa na maswali ya kuchagua huenda tukakosa ufanisi na wakafaulu kwa bahati nasibu.
C. Gharama kubwa za uendeshaji. Usaili huu unaweza kulitia hasara taifa hata ukisikiliza taarifa nyingi za CAG pesa nyingi zinapotea kupitia mifumo hewa(vassal systems) kama hii ambapo sasa gharama kubwa zinatumika katika uendeshaji hali ya kuwa idadi inayotakiwa ni ndogo.
D. Utaratibu huu wa usaili umeenda kinyume na taratibu zilizopita ambapo katika kanuni za Utumishi wa kada ya ualimu unaelekeza baada ya kumaliza ngazi husika ya ualimu hatua inayofuata ni kusubiri kupangiwa vituo vya kazi haya mabadiliko ilibidi yawekwe kwenye dira ya maendeleo 2025-2050. Ili miaka ishirini na sita ijayo ndio huu utaratibu wa usaili uanze.
WITO: Serikali ya Mama Yetu Mh. Rais Dkt. Samia Suluh Hassan, ni sikivu na inafuatilia kwa ukaribu wananchi wake na kazi kubwa inaendelea kila mtu ni shahidi, hivyo hatma ya ajira za ualimu zitawekwa sawa kupitia ushirikishwaji wa wataalamu mbalimbali na wadau wa elimu nchini.
MAMA SAMIA, MITANO TENA.
Ahsante sana.