Ligi Kuu Ya Africa Kusini Na Maajabu Yake

Ligi Kuu Ya Africa Kusini Na Maajabu Yake

Revoo

Member

Reputation: 22%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
192
Ukifatalia kwa ukaribu ligi kuu nchini Afrika kusini PSL utapata kufahamu vilabu na madaraja yake kama vile vigogo( Orlando Pirates, Kaizer na Mamelodi Sundowns)

Halikadhalika kuna zile timu za wastani daraja la kati zenyewe zipo kwa ajili ya kupambania nafasi za kati au hata kufanikiwa kuingia nafasi mbili za juu kwa maana 2 na 3.

Aina ya daraja hili utazikuta timu nyingi kama Cape Town City ambayo kwenye ligi ya PSL ni aina ya timu ya daraja hilo au chini yake.

Mara zote hazipambanii ubingwa ila kuna lengo la kukusanya alama na kusalia kwenye nafasi nzuri mwisho wa msimu.

Pia, miongoni mwa malengo ni kuvivuluga hivi vilabu vikubwa vinavyopambania ubingwa, kung'ang'ania alama au walau alama moja pindi zipocheza.

Hapana nazungumzia PSL huko Bondeni kwa Madiba kuna timu inaitwa CAPE TOWN CITY, ndani ya wiki moja imekutana na Kaizer Chiefs na Orlando Pirates na kufanikiwa kusepa alama zote 6.
FB_IMG_1736430334957.webp

Cape Town City 1-0 Kaizer Chiefs

Cape Town City 1-0 Orlando Pirates

Cape Town City siku zote imekuwa ni kisanga kwa Vigogo.
 
Back
Top Bottom