Wasailiwa mnaarifa kuwa, kuna mabadiliko ya ratiba au mahali pa usaili kwa kada zote za NECTA, baadhi ya kada za MDA’s & LGA’s pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili kama inavyoonekana hapa chini;-
- Usaili wa vitendo na mahojiano kwa kada zote za NECTA umesogezwa mbele hadi tarehe 20 - 21 Mei 2025.
- Usaili wa mahojiano kwa kada ya ‘Medical Officer II’ – Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) utafanyika tarehe 6 Mei, 2025.
- Usaili wa Mahojiano kwa kada ya ‘Msaidizi wa Kumbukumbu II’ – MDA’s & LGA’s umesogezwa mbele hadi tarehe 18 Mei, 2025 na utafanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma
- Usaili wa mahojiano kwa kada ya ‘Afisa TEHAMA Msaidizi II’ – MDA’s & LGA’s utafanyika katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira kwa tarehe zilizopo katika tangazo la kuitwa kwenye usaili.
Nafasi za SUMAIT Tanzania
28-04-2025