Mabadiliko ya Tarehe za Usaili kwa Kada Mbalimbali Ajira Portal Waombaji kazi wote walioitwa kwenye usaili wa kuandika kwa njia ya mtandao kwamwezi Machi 2025, wanajulishwa kuwa kuna mabadiliko ya tarehe za usaili kwa baadhiya kada.Mabadiliko hayo yameoneshwa kwa waombaji kazi wote ambao tarehe zao zausaili zimebadilika.Hivyo; waombaji kazi wote wanatakiwa kuzingatia ratiba inoyoonekana kwenye akauntizao za Ajira portal.Aidha, waombaji kazi wote walioitwa kwenye usaili wanakumbushwa kuzingatia mudana vituo vya usaili wa kuandika kwa njia ya mtandao kama vilivyooneshwa kwenyeakaunti zao.Ili kuona ratiba na taarifa zaidi tembelea tovuti yetu ajira.go.tz au piga simuhuduma kwa wateja namba: 026 2160350.