Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025/2026 Chuo cha Uhamiaji

Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025/2026 Chuo cha Uhamiaji Idara ya Immigration

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi.
Orodha ya majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025/2026 kuitwa immigration Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia Vijana waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kuripoti Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga, kilichopo Boma Kichakamiba, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga, kwa kuzingatia ratiba ifuatayo:
Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025/2026 Chuo cha Uhamiaji

  • Tarehe ya Kuripoti: Jumamosi, 01 Machi 2025
  • Muda wa Kuripoti: Saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana
  • Angalizo: Atakayeripoti baada ya muda uliotajwa hatapokelewa.
Kwa walioomba na kuchaguliwa kupitia Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kuripoti kwa ratiba ifuatayo:
  • Mahali pa Kuripoti: Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (Tunguu)
  • Tarehe ya Kuripoti: Jumatatu, 24 Februari 2025
  • Muda wa Kuripoti: Saa 2:00 asubuhi
2. Nyaraka za Kujiunga na Chuo
Mwanafunzi anatakiwa kuripoti akiwa na vyeti halisi vya elimu na fani mbalimbali. Mwanafunzi ambaye hatawa na nyaraka halisi hatapokelewa chuoni. Nyaraka zinazotakiwa ni kama ifuatavyo:
Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 20252026 Chuo cha immigration

  1. Cheti cha kuzaliwa
  2. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba
  3. Vyeti halisi (Original) vya Elimu ya Kidato cha Nne, cha Sita, na Shahada
  4. Vyeti vya Ujuzi wa aina mbalimbali (kwa wale wenye ujuzi)
3. Vifaa na Mahitaji ya Kujiunga na Chuo
Mwanafunzi anatakiwa kuja na vifaa na mahitaji yafuatayo:
  • Fedha:
    • Tshs. 50,400/= kwa ajili ya Bima ya Afya (kwa asiye na Kadi ya Bima ya Afya au mwenye kadi inayomaliza uhai wake kabla ya tarehe 31/12/2025)
    • Tshs. 25,000/= kwa ajili ya vipimo vya afya
    • Fedha za kujikimu kwa matumizi binafsi
  • Mavazi na Vifaa:
    • Truck suit (02) – rangi nyeusi na dark blue
    • Raba za michezo jozi (02) – rangi yoyote
    • Nguo nadhifu za kiraia jozi (03)
    • Mashuka (04) – rangi ya bluu
    • Mto wa kulalia (01)
    • Foronya (02) – rangi ya bluu
    • Chandarua (01) – rangi ya bluu
    • Madaftari makubwa (04) – 4QRs
    • Sanduku la chuma (Trunker)
    • Ndoo za plastiki (02) – moja ya lita 10 na moja ya lita 20
    • Fulana (02) – rangi ya dark blue zenye shingo ya duara
    • Viatu vya mvua (rainboot) jozi (01)
    • Taulo (01)
    • Kandambili jozi (01)
  • Vifaa vya Usafi:
    • Jembe (01) na mpini wake
    • Fyekeo (01)
    • Panga (01)
    • Rake (01)
Angalizo: Vifaa vilivyotajwa vinapatikana katika Duka la Chuo, hivyo mwanafunzi anaweza kuvinunua kwa ridhaa yake.

4. Angalizo Muhimu
  1. Gharama za usafiri kutoka nyumbani kwenda chuoni zitagharamiwa na mwanafunzi mwenyewe.
  2. Waliochaguliwa kujiunga na mafunzo watafanyiwa uchunguzi wa afya kabla ya kuanza mafunzo. Wale watakaobainika kuwa na changamoto za kiafya hawataruhusiwa kujiunga na Chuo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo.
5. Orodha ya Majina
Orodha ya majina ya walioitwa kwenye mafunzo inapatikana kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji: www.immigration.go.tz.

Bonyeza hapa ku-download majina

Imetolewa na:
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
06 Februari 2025
 
Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom