Matokeo Ya Mechi: Mc Alger 1 Vs 0 Tp Mazembe Michuano Ya Klabu Bingwa Africa TotalEnergies CAFCL

Matokeo Ya Mechi: Mc Alger 1 Vs 0 Tp Mazembe Michuano Ya Klabu Bingwa Africa TotalEnergies CAFCL 2024/2025

Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.
Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.

Revoo

Member

Reputation: 22%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
194
MC Alger ushindi muhimu sana kwao katika harakati za kutinga robo fainali, wamestahili alama 3 dhidi ya TP Mazembe kwa ustadi mzuri wa utendaji, Pointi nane kabatini kwa MC Alger
-qca6lk.webp


Tp Mazembe walikuwa na muundo wa 4-1-4-1 wakiwa na mpira ili kutengeneza usawa mzuri katika kuzuia na kushambulia ‘Balance’ lakini wakashindwa kuzingatia SPACE na DISTANCE katika nyakati sahihi na ikawa inawapa ugumu kuzuia kwa usahihi hasa wakipoteza mali

MC Alger waliingia na muundo wa 3Box Midfield3 lengo lao ni kuwa spare man zaidi katikati ya uwanja ambapo Akram Bouras na viungo wenzake watatu, na wakaanza kuutawala mchezo kwasababu walikuwa na idadi kubwa ya wachezaji katikati ‘ Numerical superiority’

Pia MC Alger wakaanza kudumisha kuwa finyu / kubana zaidi , kutoka mstari wa ulinzi hadi kiungo umbali ni mdogo na kutoka katika kiungo hadi katika ushambuliaji umbali mdogo, ongeza nafasi ya mchezaji mmoja hadi mchezaji mwingine ni ndogo sana

TP Mazembe kitu cha Space na Distance kilikuwa viseversa kwao ndio maana ilikuwa inawapa shida sana kuzuia yani wapo mbali mbali na kuifungua defense ya MC Alger ilikuwa ni ngumu kwasababu walikuwa compact kweli kweli , hapo iliwahitaji MC Alger kuwasababisha TP Mazembe kufanya mistakes kwa kukaa zaidi na mali

Hilo liliwalipa MC Alger , na kwa namna TP Mazembe walikuwa wakicheza wangeweza kuokota hata mbili au tatu wavuni why ? Runs zao nyuma ya walinzi na kiungo cha MC Alger zilikuwa dhaifu sana , kushindania mipambano yao mingi walishindwa na decisions making zilikuwa za hali ya chini

Halainini ni bonge moja la beki wa kulia anapanda na kushuka kwa wakati sahihi na nyakati sahihi ‘mithili ya Kapombe / Trent Anord’ , Akram Bouras ndio muhimili mkubwa zaidi wa MC Alger anaamua timu icheze vipi aisee , Traore pasi zake nyingi hazikuwa sahihi

Meziani ni msumbufu sana na yupo strong Bongeli ni mchezaji mzuri sana aisee Gk wa MC Alger anafika katika actions / mpinzani kwa wakati sahihi kuondoa hatari

FT: MC Alger 1-0 TP Mazembe
FB_IMG_1736566880504.webp
 
Back
Top Bottom