Lucy Benjamin
New member
Mafanikio ya mwanafunzi yanaweza kueleweka kama uwezo wa mwanafunzi kufikia malengo yake yakujifunza na kukuza ujuzi muhimu kwa maisha ya baadae.asilimia kubwa ya wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu uweka juhudi nyingi katika kusoma na kufaulu mitihani yao wakiwa na imani kuwa hatma ya mafanikio yao iko katika ufaulu wa mitihani hiyo.
Matokeo hayo hutumika kupima ujuzi wa mwanafunzi katika nafasi fulani ya kazi mara baada ya kuhitimu. Matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne na sita pamoja na chuo kikuu upewa kipaumbele katika kuangalia vigezo mbalimbali pale anapoenda kuomba kazi sehemu fulani.
Mwanafunzi anabidi kuelewa kuwa matokeo ya mitihani sio njia pekee ya kupima mafanikio yake bali zipo njia mbali mbali zinazoweza kutumika kupima mafanikio kama vile ushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo michezo, vilabu vya shuleni au vyuoni, miradi ya kijamii, ambayo husaidia kujenga ujuzi mbalimbali kama akiba ya maisha baada ya kuhitimu.
Pia ushirikiano na wenzake ni kipimo kingine cha mafanikio ya mwanafunzi ambapo uwezo wake wakuleta mawasiliano mazuri baina yake na wenzake ujenga ushirikiano wenye kuleta maendeleo yake binafsi pamoja na jamii inayozumzunguka. Hii huenda sambamba na maendeleo binafsi ya mwanafunzi yanayohusisha akili, hisia na jamii. Mwanafunzi anaejitambua ni rahisi kufanikiwa na kuendelea.
Moja ya mambo muhimu katika mazingira ya kazi na jamii, uhitaji ujuzi na ubunifu, ushirikiano, mawasiliano. Mitihani mingi huwa na muundo rasmi na pendekezi ambao ni wa kawaida na unambana mwanafunzi kuonyesha ubunifu wake. Mwanafunzi anaweza kuwa na uwezo na mawazo mazuri lakini muundo wa maswali kuwa wa moja kwa moja ukamfunga.
Serikali imelitambua hilo nakuruhusu mabadiliko ya mitaala ya elimu,ili kukidhi mahitaji ya soko na jamii.Pia matumizi ya vifaa vya kielektroniki na programu za kujifunzia ambazo zinaboresha ufundishaji na ujifunzaji unaohusisha walimu pamoja na wanafunzi.
Hatua hizi zimepelekea mfumo wa elimu kuwa bora zaidi yenye kutoa ujuzi na maarifa yenye kuleta tija katika jamii na maisha yao binafsi kwa sasa na baadae.
Mwanafunzi anapaswa kujitathmini na kujifunza kutokana na makosa yake ili kuboresha uwezo wake. Mwelekeo wake binafsi na utayari wa kujifunza na kusonga mbele unamtengenezea nafasi ya kufikia malengo na kufanya kazi kwa bidii ili kuyatimiza. Matokeo ya mtihani mmoja isiwe sababu ya kukata tamaa bali ni daraja na ngazi ya yeye kusonga mbele.