Mkutano Na Waandishi Wa Habari Nchini Tunisia, Simba Sports Club Kuelekea Mchezo Wa Leo January 05, 2025 CAFCC

Mkutano Na Waandishi Wa Habari Nchini Tunisia, Simba Sports Club Kuelekea Mchezo Wa Leo January 05, 2025 CAFCC

Revoo

Member

Reputation: 19%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
169
Kocha Mkuu wa klabu ya Simba sports club Fadlu Davids ameweka wazi kuwa mchezo wa leo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika (๐—ง๐—ผ๐˜๐—ฎ๐—น๐—˜๐—ป๐—ฒ๐—ฟ๐—ด๐—ถ๐—ฒ๐˜€๐—–๐—”๐—™๐—–๐—–) dhidi ya CS Sfaxien utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani

Kocha Fadlu amesema pamoja na CS Sfaxien kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi la kumfuta kazi kocha wao lakini bado wana timu imara ambayo inaundwa na vijana pamoja na wazoefu.
FB_IMG_1736054608224.webp

Akizungumzia kuhusu kikosi cha Simba sports club, Fadlu amesema wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa leo huku malengo yakiwa kuhakikisha pointi tatu zinapatikana

โ€œUtakuwa mchezo mgumu, ikifika hatua hii kila mchezo unakuwa mgumu hasa ukiwa ugenini lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo chanya,โ€ amesema Kocha Fadlu.

Kwa upande wake mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa kupata ushindi kwenye mechi ya leo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.

โ€œTunajua tupo ugenini na haitakuwa mechi nyepesi lakini tumejiandaa vizuri na tupo tayari kwa Mapambano,โ€ amesema Che Malone.

Mchezo Huo utapigwa leo saa moja usiku kwa saa za Tanzania katika Uwanja wa Olympique De R โ€“ Tunis.
 
Back
Top Bottom