Ndugu wananchi Forum, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Geita anapenda kuwataarifu wananchi wote wenye sifa, nafasi Arobaini (40) za Ajira ya Mkataba ya ukusanyaji Mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ajira mpya za Kukusanya Ushuru December 2024.
Maombi yote yapelekwe:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Geita,
S.L.P. 139,
GEITA.
Sifa za mwombaji
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe amehitimu Kidato cha Nne na kuendelea.
- Awe na nidhamu nzuri yenye kujituma na kuwajibika.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi ngumu ikiwemo hata Mahakamani.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kujituma bila kusimamiwa.
- Awe tayari kufanya kazi katika Kata yoyote kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
- Awe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.
Kazi na majukumu
- Kukusanya Mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mambo ya Jumla ya Kuzingatia
- Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne na kuendelea.
- Waombaji waambatanishe CV na Vyeti vya Elimu vilivyothibitishwa na Wakili, Mwambie Brashi (CV), Nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
- Katika barua ya maombi, weka namba yako ya simu inayopatikana muda wote.
- Barua zibandikwe picha ndogo (2) - Passport size.
- Barua ziambatanishwe na majina ya watu wawili wanaoelezea tabia na usuli.
- Maombi yote yaambatanishe na barua za Wadhamini Wawili zinazoonesha mahali anapoishi mwombaji.
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/12/2024 saa 9:30 alasiri.
Maombi yote yapelekwe:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Geita,
S.L.P. 139,
GEITA.