Huduma za Afya za Aga Khan, Tanzania (AKHST), taasisi ya Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, ilikamilisha awamu ya pili ya upanuzi mkubwa wa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam mwaka 2018. Upanuzi huu ulilenga kuboresha ubora wa vifaa na miundombinu ya hospitali hiyo ili kuwa kituo cha kisasa chenye vitanda 170, kwa ajili ya kuongeza uwezo wake kama mtoa huduma za afya za hali ya juu, kituo cha rufaa, na hospitali ya kufundishia.
Attachments