NHIF YAZINDUA MFUMO NA KIFURUSHI CHA TOTO AFYA KADI (TAK)

NHIF YAZINDUA MFUMO NA KIFURUSHI CHA TOTO AFYA KADI (TAK)

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 100%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
1,640
LEO: Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) anatarajia kuzindua Mfumo wa uandikishaji Wanachama, Mfumo wa Uchakataji Madai na Kifurushi cha Toto Afya Kadi Desemba 17, 2024. Uzinduzi wa Mfumo unafanyika baada ya Mfuko kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha Mfumo wa Serikali inasomana.

Aidha kwa upande wa Toto Afya Kadi, Mfuko umefanya marejeo ya kifurushi hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kundi la watoto chini ya umri wa miaka 18, hali ya kipato cha wananchi pamoja na hali ya Mfuko. Kutokana na hayo, mpango huo wa Toto Afya Kadi utazinduliwa rasmi kwa tarehe tajwa hapo juu.

Kwa sasa Mfuko unaendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote hususan katika usajili wa wanachama kupitia makundi mbalimbali ikiwemo kundi la Wanafunzi kuanzia ngazi ya Awali hadi Chuo Kikuu kwa gharama ya shilingi 50,400/= tu.
NHIF YAZINDUA MFUMO NA KIFURUSHI CHA TOTO AFYA KADI (TAK)

Mfuko unatoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu wakati wowote bila kikwazo cha fedha kupitia mtandao mpana wa vituo zaidi ya 10,000 vya kutoa huduma nchi nzima.

Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano kwa Umma
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)
 
Similar content Most view View more
Back
Top Bottom