Ratiba ya Mapinduzi Cup 2025

Ratiba ya Mapinduzi Cup 2025

Revoo

Member

Reputation: 18%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
160
Michuano ya Mapinduzi Cup 2025 inatarajiwa Kuanza rasmi January 03,2024 huku Fainali zikitarajiwa kufanyika January 13,2024.

Droo ya kupanga Makundi itafanyika kwenye Uwanja wa Gombani Pemba, ambao utatumika kama uwanja wa mashindano baada ya uwanja wa Amaan kuwa kwenye maboresho.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Bw Suleiman Jabir, mashindano hayo yatahusisha timu za taifa kutoka Zanzibar, Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na Burkina Faso.

Timu hizo zitagawanywa katika Makundi mawili, ambapo timu mbili Bora kutoka kila Kundi zitafuzu hatua ya Nusu Fainali, na baadae, washindi watakutana katika Fainali.
images-37-9.jpeg.webp


Bingwa wa mashindano hayo haya ataondoka na zawadi ya Shilingi Milioni 100.

Katika hatua nyingine, kamati ya maandalizi ya mashindano hayo imepanga kutoa sapraizi na zawadi mbalimbali kwa mashabiki na wachezaji.

Jabir alibainisha kuwa kutakuwa na tuzo za wachezaji mmoja mmoja katika vipengele mbalimbali, na mipango ya kuongeza vionjo vya kipekee kwenye mashindano haya imekamilika.

Timu Zitakazoshiriki Mapinduzi Cup 2025

Timu za taifa zilizothibitishwa kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup 2025 ni:

Zanzibar Heroes
Kenya
Uganda
Kilimanjaro Stars (Tanzania)
Burundi na
Burkina Faso
 
Back
Top Bottom