What's new

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Wametangaza Ajira Mpya 25 Kwa Watanzania

Sia

Member
Tanzania: Kwa niaba ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawaalika Watanzania wenye uzoefu, wenye bidii, wabunifu, na waliohitimu vigezo vinavyofaa kujaza nafasi ishirini na tano (25) za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni Shirika la Utangazaji la Umma lililoanzishwa kwa Amri ya Serikali mwaka 2007 na kuanza rasmi shughuli zake tarehe 1 Julai 2007, likichukua nafasi ya Tanzania Broadcasting Services – Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT). TUT ilianzishwa mwaka 2002 kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma Na. 2 ya mwaka 1992, Tangazo la Serikali Na. 23 la tarehe 14 Juni 2002. Kuundwa kwake kulikuwa ni matokeo ya muunganiko wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) iliyoanzishwa mwaka 1972 na Televisheni ya Taifa (TVT) iliyoanzishwa mwaka 1999.

 
Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. S.L.P 2320, Jengo la Utumishi, Chuo Kikuu cha Dodoma – Majengo ya Dr. Asha Rose Migiro - Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 4 Novemba, 2024.
 
Jinsi ya kujisajili na kutuma maombi Ajira Portal katika nafasi za kazi 25 TBC

Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia Mfumo wa Ajira kwa kutumia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ na si vinginevyo (Anuani hii pia inaweza kupatikana kwenye Tovuti ya PSRS, Bonyeza ‘Recruitment Portal’).
 
Back
Top