TETESI LEO: Usajili wa Feisal Salimu Kwenda Simba, Mazungumzo Yafanyika

TETESI LEO: Usajili wa Feisal Salimu Kwenda Simba, Mazungumzo Yafanyika

Hatua za Kuuliza swali. Anza na Title ya swali kisha Chini yake weka maelezo kuhusu swali lako.
NB: HATUJIHUSISHI NA VITU VINGINE ISIPOKUWA AJIRA.
Bonyeza hapo kujiunga nasi kupata matangazo mbalimbali ya kazi, Maswali ya Usaili.

Sia

Moderator

Staff member
Reputation: 89%
Joined
Oct 20, 2024
Messages
792
Kiungo mahiri wa mpira kutoka Zanzibar, Feisal Salum Abdalah, maarufu kama Fei Toto, ameonyesha dalili za kuachana na Azam FC, klabu aliyokuwa akiitumikia kwa muda sasa. Japokuwa uongozi wa Azam umejaribu kumshawishi aongeze mkataba wake unaoisha mwakani, Feisal anaonekana kutamani changamoto mpya nje ya klabu hiyo.
TETESI LEO: Usajili wa Feisal Salimu Kwenda Simba, Mazungumzo Yafanyika

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Feisal, kiungo huyo anakaribia kujiunga na Simba SC ya Kariakoo, Dar es Salaam. Anasubiri Simba na Azam wakamilishe makubaliano katika dirisha hili dogo la usajili ili aweze kuvaa jezi za Msimbazi. Inaonekana Simba ndiyo timu anayotaka kuichezea kwa sasa, na ana imani kuwa itampa nafasi ya kung'aa zaidi na kujulikana barani Afrika.

Chanzo hicho kinasema Feisal ana matumaini makubwa na malengo ya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotambulika sana barani Afrika. Anaamini kupitia Simba, atapata nafasi ya kuonyesha kipaji chake kwenye mashindano makubwa na kukua zaidi katika soka.

Iwapo uhamisho huu utakamilika, Simba SC itapata kiungo hodari mwenye uwezo wa kuongoza mashambulizi na kasi ya hali ya juu. Kwa upande wa Feisal, ni nafasi nzuri kwake kupiga hatua mbele na kuendeleza ndoto yake ya kucheza soka la kimataifa.
 
Back
Top Bottom