Tubuni Mkiwa Hai Bado Kwa Shomari Kapombe Wa Wekundu Wa Msimbazi

Tubuni Mkiwa Hai Bado Kwa Shomari Kapombe Wa Wekundu Wa Msimbazi

Revoo

Member

Reputation: 21%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
182
Zilipita Zilikuwepo na zikaondoka kwenye Ardhi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K Nyerere namba 2 bora sana Lakini hakuna aliyetikisa hata nusu ya Uwezo wa Shomari Kapombe.
FB_IMG_1736283215058.webp

Ndani ya Ardhi hiii Hakuna namba 2 aliyewahi kucheza Katika Kiwango Bora kwa Zaidi ya Misimu 9 bila kushuka Kiwango chake zaidi ya Shomari Kapombe pekee.

Kijana aliyesimama katika ubora huu hadi sasa amekuwa Beki namba Mbili wa kutegemewa Ndani ya Kikosi cha Simba..

Pale Al Ahly yupo Al Maaloul Misimu wake wa 11 katika ubora wake.

Simba wana Shomari Kapombe Zaidi ya Misimu 9 Katika ubora wake.

Miguu ya Mageiji wa soka akina Ivanoviç Klosi za Solomon Kalou, Mikimbio ya James Milner.

Rudi katazame Clip za Ivanoviç akiwa darajani nenda kamwangalie Dribling za Solomon Kalou akiwa anamtafuta Nicklaus Enelka,Frank Lampard sambamba na Didier Drogba.

Tena rudi unyamani mtazame Mr water Pump Shomari Kapombe akifanya international dribbling Kabla ya Kumwaga Maji kuelekea kwa Ateba Ahoua sambamba na Kibu Denis Prosper.

Kama hujawahi kuinjoy soka La Shomari Kapombe basi acha mpira fani hii umevamia nenda kamshabikia Undertaker huko WrestleMania WWE.
FB_IMG_1736064564482.webp

Huyu Mr water Pump Shomari Kapombe Kaletewa Mabeki Wengi Sana kutoka..
  • Congo
  • Ivory Coast
  • Ghana
  • Nigeria
  • Mali

Wakamfananisha nae hadi wengine wakataka kumshusha Heshima yake kwenye soka kwa kuwapa vipaumbele wachezaji wao waonekane Bora Zaidi

Lakini mwamba imara...Umesimama kama mnara wa Baberi hakuna wakuushusha.

Huyu Ndiye Shomari Kapombe aliyesimama mithiri ya kilele cha Mawenzi pale Kilimanjaro Mount.

SI Kuna muda mnatakiwa kutubu.

Bali ni Muda wa kutubu ya kuwa Shomari Kapombe is incomparably in East and Central Africa.

Apewe maua yake.
 
Back
Top Bottom