Wachezaji Wazawa Tanzania Wanaweza Waaminiwe

Wachezaji Wazawa Tanzania Wanaweza Waaminiwe

Revoo

Member

Reputation: 18%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
160
Pichani ni Abdulrazak Hamza na Yusuph Kagoma wachezaji wa Simba Sc wenye utambulisho wa uraia wa Tanzania.
FB_IMG_1736182406575.webp


Ni sajili za dirisha kubwa la usajili msimu wa 2024/25 pale Lunyasi.

Naamini asilimia kubwa ya watanzania wakati wa sajili hizi waliamini/tuliamini ni wachezaji wa ziada kwenye timu kutokana na mahitaji ya Simba Sc.

Ipo wazi huwa tunaamini zaidi wachezaji wa kimataifa kuliko wa kizawa linapokuja swala la Simba na Yanga Sc.

Ila mambo yakaamua tofauti kabisa, wale wachezaji wa kimataifa wanakaa mbao ndefu halafu Hamza na Kagoma wanaaanza na wanatoa ubora wa juu sana.

Wachezaji wetu wengi wa kizawa wanafichwa na kivuli cha wachezaji wa kimataifa, kwasababu makocha wengi hawatoi nafasi hiyo kwasababu wazijuazo wenyewe, ila Fadlu Davids ametoa picha halisi ya kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza na kuonesha alichonacho.

Ndio maana Hamza anaanza mbele ya Karobue Chamou.

Ndio maana Yusuph Kagoma anaanza mbele ya Augustine Okejepha, sio kwa upendeleo bali uwezo wa kutimiza majukumu yao kwa ubora wa juu.

Pengine Katika dirisha kubwa la usajili wa 2024/25 ndani ya Simba Sc Yusuph Kagoma ndio sajili bora zaidi kwa local players halafu anafuata Abdulrazak Hamza.

Yusuph Kagoma ni picha halisi ya kiungo cha ulinzi ambacho Simba Sc walikikosa baada ya wachezaji kama James Kotei, Fraga Viera na Thadeo Lwanga kuondoka ndani ya Simba Sc.

Najua kuna watu watauliza mbona hujataja jina la Jonas Mkude? Simple answer ni kwamba Jonas Mkude sio/hakua kiungo mkabaji kiasili ndani ya Simba Sc, yeye ni holding midfielder.

Naamini kama makocha weupe wakiendelea kutoa nafasi bila kuangalia huyu ni mzawa au mchezaji wa kimataifa basi kuna wachezaji wengi wa kimataifa watasugua mbao ndefu.

Shida ni kwamba hao wa kimataifa wanawalipa pesa nyingi kwahiyo huwa wanaona sio poa muda mwingi kukaa mbao ndefu, ndio wanawapangia kikosi makocha.

NOTE:

1. Wachezaji wazawa wanaweza ni basi tu trust imekua ndogo kwao.

2. Kuna magarasa mengi ya kimataifa yanazidiwa uwezo na local players.

Uzuri mifano ipo.
 
Back
Top Bottom