Wasailiwa wa Ajira za TRA Watakaofanya Vizuri kuhifadhiwa kwenye kanzi data

Wasailiwa wa Ajira za TRA Watakaofanya Vizuri kuhifadhiwa kwenye kanzi data 12-05-2025

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema wasailiwa watakaofanya vizuri katika Usaili wa mahojiano watahifadhiwa kwenye kanzi Data ya TRA na kuajiriwa pale patakapokuwa na upungufu wa Watumishi kutokana na sababu mbalimbali.
Wasailiwa wa Ajira za TRA Watakaofanya Vizuri kuhifadhiwa kwenye kanzi data

Amesema hayo leo tarehe 12.05.2025 alipotembelea zoezi la Usaili wa mahojiano kwa waombaji wa nafasi za Tax Management Officer II, Economist II, Statistician II, Assistant Lecturer, Librarian II, Warden II, Academic Officer II, Tutorial Assistant na Laboratory Officer II kwenye eneo la APC Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Amesema wote waliofika hatua ya usaili wa mahojiano wana uwezo lakini hawawezi kuchukuliwa wote kutokana na uchache wa nafasi zilizopo ambazo ni 1,596.

"Najua haikuwa rahisi kufika hapa mlipofika, nawapongeza sana, wote mtakaofanya vizuri tutawaweka kwenye kanzi Data yetu, wakati mwingine tukihitaji kuajiri tutachukua hapo, hakutakuwa na haja ya kupitia mchakato mrefu hasa pale Watumishi wanapostaafu" amesema Mwenda.

Amewahakikishia wote wenye uwezo kuwa wataajiriwa kutokana na uwezo wao ndiyo maana amekwenda kujiridhisha ili kuona haki inatendeka kwenye Usaili wa mahojiano.
 
Similar content Most view View more
Back
Top Bottom