Yanga Kufuatia Mchezo Wa Kesho January 04, 2025 Dhidi Ya Tp Mazembe Nyumbani (CAFCL)

Yanga Kufuatia Mchezo Wa Kesho January 04, 2025 Dhidi Ya Tp Mazembe Nyumbani (CAFCL)

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026

Revoo

Member

Reputation: 22%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
194
Ni kweli Yanga ni miongoni mwa timu 6 ambazo hazijafanikiwa kupata ushindi wowote kwenye michuano ya CAF Interclub.
FB_IMG_1735896464658.webp

Ni kweli Yanga wana alama moja mkiani.

Lakini, Sidhani kama Yanga wakishindwa kufuzu hatua ya robo fainali ikuwa story kubwa sana...Na sioni kama kuna ulazima wa matokeo hayo kama yatatokea kuwaumiza kwa muda mrefu.

Kwenye Football kuteleza kupo, Kwenye mpira huku sio kila timu inayopata matokeo uwanjani inakuwa bora kwa wakati huo.

Yanga wasipofuzu hatua ya robo fainali mwaka huu haitaondoa ubora na mafanikio yao waliyoyapata hivi karibuni kwenye michuano hiyo.

Haitaficha ukweli kwamba Yanga walifika fainali ya Kombe la Shirikisho tena kwa kushinda ugenini mbele ya maelfu ya mashabiki na moshi mwingi uwanjani.

Haitafuta ubora wao kwenye mechi mbili za robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye ligi ya Mabingwa.

Na haitaondoa ukweli wa utawala wao kwa soka la ndani kwa misimu mitatu mfululizo...

Nataka kusema nini...?

Kuelekea kwenye mchezo wa kesho wa Yanga vs Tp Mazembe kila mtu ndani ya Yanga anatakiwa kufanya sehemu ya majukumu yake...

Sead Ramovic aandae timu, Viongozi wafanye kwa upande wao na mashabiki wajae uwanjani!

Kusiwepo ahadi na vikao vingi vikawapa presha kubwa wachezaji wakashindwa kufanya kazi yao bora kiwanjani.

Inawezekana kushinda bila ahadi nyingi...
Inawezekana kushinda bila Tambo nyingi...

Kila la heri wananchi.
 
Back
Top Bottom