Hizi hapa hatua, Jinsi ya Kuhama kama Mtumishi wa Umma kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine | TAMISEMI 2024/25 au Utumishi
Soma zaidi: Uhamisho wa Watumishi wa Umma 2024
Mamlaka za Uhamisho
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni za mwaka 2003, Mamlaka za Uhamisho ni kama ifuatavyo:- Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Mamlaka ya jumla ya uhamisho.
- Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI: Uhamisho wa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa.
- Katibu Tawala wa Mkoa: Uhamisho ndani ya Mkoa, baina ya Halmashauri.
- Mkurugenzi wa Halmashauri: Uhamisho ndani ya Halmashauri moja, kutoka kituo kimoja kwenda kingine.
Aina za Uhamisho
Kuna aina mbili kuu za uhamisho kwa watumishi wa umma:1. Uhamisho wa Kuomba
Watumishi wanaweza kuomba uhamisho kwa sababu maalum. Hapa ni hatua na taratibu za kufuata:- Maombi ya Uhamisho: Mtumishi atawasilisha ombi lake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri anakotaka kuhamia, kupitia kwa msimamizi wake wa kazi.
- Usimamizi wa Maombi: Wasimamizi wa mtumishi wana wajibu wa kuhakikisha maombi hayo yanafika kwa mamlaka husika kwa usahihi na bila vizuizi visivyo na sababu.
- Mchakato wa Rufa: Ikiwa ombi limekataliwa na mtumishi hakuridhika, anaweza kuwasilisha ombi kwa Katibu Tawala wa Mkoa na kama bado hakuridhika, anaweza kufikisha kwa Katibu Mkuu TAMISEMI kwa rufaa.
- Sababu za Kupewa Gharama za Uhamisho: Watumishi wanaohama kwa sababu ya kumfuata mume/mke au baada ya kukaa muda mrefu nje ya mkoa wanaweza kugharamiwa.
- Majibu ya Maombi: Majibu hutumwa kwa waajiri na hutangazwa kwenye tovuti ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).
2. Uhamisho wa Kawaida
Uhamisho huu unafanywa na mwajiri kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa kazi. Kwenye aina hii ya uhamisho:- Mamlaka za uhamisho hujiridhisha kuhusu uwepo wa nafasi wazi na uwezo wa kugharamia uhamisho.
- Uhamisho unaweza kufanyika wakati wowote inapohitajika ili kuboresha huduma za umma.
Taratibu Muhimu za Kufuata
Upatikanaji wa Majibu
Watumishi wote walioomba uhamisho watapata majibu kupitia kwa waajiri wao. Majibu haya hupatikana kupitia tovuti ya TAMISEMI mapema Julai na Januari kila mwaka.Utaratibu wa Malalamiko
Watumishi ambao hawajaridhika na majibu ya uhamisho wanaweza kuelekeza malalamiko yao kwa mamlaka husika wakitoa sababu na vielelezo muhimu vya maombi yao.Taarifa za Kuwasilisha Maombi
Ni muhimu kuwasilisha maombi ya uhamisho mwenyewe kupitia kwa mwajiri au njia rasmi kama EMS ili kuweka kumbukumbu sahihi.Tahadhari kwa Watumishi
Watumishi hawaruhusiwi kughushi saini au kupokea rushwa katika mchakato wa uhamisho. Kitendo hiki kitachukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria.Maandalizi ya Uhamisho kwa Waajiri
Waajiri wanapaswa kuhakikisha majibu yote ya uhamisho yamefuata taratibu na kuandaa taarifa za mishahara na kumbukumbu kwa watumishi watakaojiunga.Soma zaidi: Uhamisho wa Watumishi wa Umma 2024