What's new
Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi (PSRS) 2024 | Taasisi Mbalimbali PDF leo

Ajira Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi (PSRS) 2024 | Taasisi Mbalimbali PDF leo 31 Oktoba 2024

Hii hapa orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi (PSRS) 2024 | Taasisi Mbalimbali PDF leo Tangazo la Matokeo ya Usaili kwa Waombaji Kazi PSRS 2024.

Kuitwa kazini utumishi na ajira portal
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawaarifu waombaji wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 07 December 2023 na 12 Septemba 2024 kuwa matokeo ya usaili yamechapishwa rasmi. Matokeo haya yanajumuisha waombaji waliofaulu pamoja na wale waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali na wamepangiwa vituo vya kazi kufuatia nafasi zilizopatikana.
Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi (PSRS) 2024 | Taasisi Mbalimbali PDF leo

Maagizo kwa Waombaji Waliofaulu​

Waombaji wote waliofanikiwa wanatakiwa kuchukua barua zao za kupangiwa kituo cha kazi ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya tangazo hili. Barua zinapatikana katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi. Barua ambazo hazitachukuliwa ndani ya muda uliowekwa zitatumwa kupitia anuani za posta za wahusika.
Pitia: Mabadiliko ya usaili Shirika la Reli Tanzania

Taarifa Muhimu kwa Waombaji​

Waombaji wanaotakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi wanapaswa kufika na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo yao kuanzia kidato cha nne hadi ngazi ya juu. Vyeti hivi vitahakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua rasmi za ajira. Ni muhimu kwa waombaji kufuata muda uliowekwa kwenye barua hizo ili kuepuka kuchelewa.

Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika orodha hii, tafadhali tambua kuwa hawakufaulu usaili huu. Hata hivyo, mnaweza kujaribu tena nafasi nyingine zitakapotangazwa.

Soma zaidi: Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal

Kuhusu Utumishi: Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali kilichopewa hadhi ya Idara huru kilichoundwa mahsusi kusaidia mchakato wa ajira wa wafanyakazi katika Utumishi wa Umma. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu 29(1).
Author
Gift
Downloads
1,597
Views
2,481
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Back
Top