Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi ya kazi kwa ajili ya Afisa Habari Daraja la II - ZPSE-10 (Nafasi 1 - Unguja) katika Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kuweza kujaza Ajira Mpya zilizo wazi kupitia ZanAjira.
Soma zaidi: Ajira Mpya TIE
Kuhusu ZanAjira: Tume ya Utumishi Serikalini ni taasisi huru iliyoanzishwa na Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 chini ya Kifungu cha 117, 2010 na Kifungu cha 33 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 2 ya mwaka 2011. Kimsingi, Tume hii ina jukumu la kusimamia watumishi wa umma kwa uadilifu na kufuata misingi ya Utawala Bora pamoja na kusimamia mchakato wa ajira.
Jinsi ya Kuomba
- Njia ya Maombi: Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki kupitia Mfumo wa Maombi ya Ajira (ZanAjira) unaopatikana kwenye anuani ifuatayo: https://portal.zanajira.go.tz
- Muda wa Kuomba: Kuanzia tarehe 31 Oktoba, 2024 hadi tarehe 08 Novemba, 2024.
- Tovuti Rasmi: Tangazo hili pia linapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini: www.zanajira.go.tz.
Maelekezo Muhimu
- Barua za Maombi: Zitume kupitia mfumo wa ZanAjira (kwa njia ya kielektroniki pekee) kwa anuani ifuatayo:
- KATIBU,
- TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
- S.L.P 1587,
- ZANZIBAR
- Kuweka Maelezo Sahihi: Muombaji anatakiwa kuainisha jina la nafasi ya kazi anayoiomba.
- Masharti: Maombi yanayoambatanishwa na "Progressive Report" au "Statement of Results" pekee hayatashughulikiwa.
- Msaada wa Kitaalamu: Kwa maswali au msaada zaidi, wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kwa simu namba 0773101012.