What's new
Nafasi za Kazi MUST | Ajira Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

Ajira Nafasi za Kazi MUST | Ajira Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya 01 Novemba 2024

Hizi hapa Nafasi za Kazi MUST | Ajira Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya zilizo tangazwa na Sekretarieti ya Ajira (PSRS) katika Utumishi wa Umma kwa watanzania wote wenye sifa.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kilianzishwa kutokana na mabadiliko kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) kupitia Sheria ya Vyuo Vikuu Na.7 ya mwaka 2005 na Katiba ya MUST ya mwaka 2013. Chuo hiki kina ndoto ya kuwa kitovu bora cha maarifa, ujuzi, na elimu ya vitendo katika sayansi na teknolojia.

MUST kinakaribisha Watanzania wenye sifa zinazohitajika na ari ya kufanya kazi kujaza nafasi kumi na nne (14) zilizopo.
Soma zaidi: Kuitwa kazini Geita

Mwongozo wa Kuomba Nafasi za Kazi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)​

Nafasi za Kazi MUST | Ajira Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinakaribisha waombaji wenye sifa kwa nafasi za kazi. Ili kuongeza nafasi ya kuchaguliwa na kuepuka makosa, tafadhali zingatia vigezo vifuatavyo:

1. Uraia na Umri​

  • Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.

2. Fursa kwa Waombaji Wenye Ulemavu​

  • Tunawahimiza waombaji wenye ulemavu kuomba na kubainisha hali yao kwenye mfumo wa ajira ili kuzingatiwa maalum.

3. Uzingatiaji wa Maelekezo​

  • Tafadhali hakikisha unazingatia taarifa zote zilizotolewa kwenye tangazo kabla ya kuomba.

4. Nyaraka Muhimu za Kuambatisha​

  • Nakala za vyeti zilizoidhinishwa za Shahada, Diploma, au vyeti vingine vya elimu.
  • Nakala za matokeo rasmi za masomo yako.
  • Vyeti vya Usajili na Mafunzo maalum (pale vinapohitajika).
  • Cheti cha kuzaliwa.

5. Nyaraka Zisizokubalika​

  • “Results slip” za Kidato cha Nne na Kidato cha Sita na nakala ambazo hazijakamilika hazitakubalika.

6. Picha ya Passport Size​

  • Pakia picha ya hivi karibuni ya Passport Size kwenye mfumo wa ajira.

7. Wafanyakazi wa Umma Waliopo​

  • Kama umeajiriwa kwenye Utumishi wa Umma, barua ya maombi inapaswa kupitishwa kwa mwajiri wako wa sasa.

8. Waombaji Waliostaafu​

  • Waliostaafu kwenye Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.

9. Wadhamini​

  • Taja wadhamini watatu wenye sifa pamoja na mawasiliano yao.

10. Vyeti vya Elimu kutoka Nje ya Nchi​

  • Vyeti vya mitihani ya sekondari kutoka nje ya Tanzania viidhinishwe na NECTA.
  • Vyeti vya kitaaluma vya nje ya nchi viidhinishwe na TCU au NACTVET.

11. Muundo wa Barua ya Maombi​

  • Barua yako ya maombi inapaswa kusainiwa, kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, na kuelekezwa kwa Makamu Mkuu wa Chuo, MUST, S.L.P 131, Mbeya.

12. Uteuzi na Usaili​

  • Waombaji waliochaguliwa watajulishwa tarehe ya usaili. Hakikisha mawasiliano yako yapo sahihi.

13. Taarifa Sahihi​

  • Kuwasilisha taarifa za kughushi kutasababisha hatua za kisheria.
Jisajili sasa kupitia https://portal.ajira.go.tz na ujihakikishie nafasi kwa kuzingatia masharti haya. Pia, pata taarifa zaidi kupitia tovuti yetu ya wananchiforum.com kwa mwongozo wa kina kuhusu nafasi mpya za ajira na maelekezo mengine muhimu.
Author
Gift
Downloads
366
Views
1,069
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Back
Top