Kwa Kagoma Simba sports club Wamepata Mtu

Kwa Kagoma Simba sports club Wamepata Mtu

Revoo

Member

Reputation: 20%
Joined
Dec 12, 2024
Messages
180
Yusuph Kagoma ni miongoni mwa viungo wachache wazawa wanaofanya vizuri sana kwenye Ligi kuu Tanzania Bara hasa kwenye hizi klabu kubwa.

Kagoma amekuwa nguzo kubwa na imara kwa klabu ya Simba jambo ambalo linampa urahisi zaidi kocha Fadlu wa kumtafuta pacha atakayecheza nae.

Kumuweka benchi mchezaji wa kigeni kwenye hizi timu kubwa sio jambo jepesi hadi upambane na uonyeshe uwezo wako haswa.Kagoma anapaswa kupewa sifa zake kwa upambanaji wake.

Naimani kuelekea AFCON na hasa CHAN mwakani 2025 tutakuwa na timu imara ambayo itaenda kushindana sio kushiriki kama ambavyo mara zote tumekuwa tukienda.
FB_IMG_1735468907040.webp
 
Similar threads Most view View more
Back
Top Bottom