Mwongozo wa kutuma maombi Ajira za Uhamiaji 2024/2025 | Mfumo wa Ajira Immigration. Mwombaji anatakiwa kuambatisha nyaraka kwenye mfumo wa Ajira kwa kutumia format ya PDF na picha ya mwombaji (passport size) katika format ya jpg/png. Kila nyaraka moja isizidi ukubwa wa 300Kb.
Orodha ya Nyaraka Zinazohitajika:
Kujisajili ajira za uhamiaji 2024
Soma zaidi:
Orodha ya Nyaraka Zinazohitajika:
- Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.
- Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo.
- Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono.
- Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU, wawe na barua za Utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi.
- Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika format ya jpg/png na isiyozidi 300Kb.
- Namba (index no) ya cheti cha Kidato cha Nne na Sita kwa waliohitimu kidato hicho, ambapo namba hizo zitajazwa kwenye mfumo wa ajira.
- Nakala ya vyeti vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada/Stashahada ya Juu (ikiwa inapatikana na viwe vimehakikiwa katika vyuo husika).
- Nakala ya cheti cha kuhitimu JKT/JKU (kwa walionavyo).
- Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi.
- Wasifu wa Mwombaji (CV).
Kujisajili ajira za uhamiaji 2024
Soma zaidi:
Attachments