Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo katika kampasi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya kwa masomo yatakayoanza mwezi MACHI 2025 katika ngazi za Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) na Shahada ya Umahiri (Mastesrs Degree). Mfumo wa ufundishaji utakuwa ni usomaji kwa njia ya Mtandaoni (Online Learning System).