- Joined
- Dec 12, 2024
- Messages
- 180
KAMA kuna kitu ambacho mashabiki na wapenzi wa Yanga wanaomba kwa leo ni kuona timu hiyo inazinduka na kupata ushindi ikiwa ugenini dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Ndio, ebu uangalie msimamo wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika inayoendelea kwa sasa, kule mkiani ndiko maskani ya Yanga ikizibeba timu zingine tatu zilizopo kundini wakiwamo vinara Al Hilal ya Sudan yenye pointi sita, MC Alger ya Algeria yenye pointi nne na Mazembe ikiwa na alama moja.
Yanga inaburuza mkia ikiwa haina pointi hata moja wala bao lolote na leo kuanzia saa 10:00 jioni itakuwa kwenye Uwanja wa Mazembe kukabiliana na wenyeji hao, huku ikiwa haina namna isipokuwa kushinda.
Matokeo ya mechi mbili za awali, Yanga ilipoteza nyumbani mbele ya Al Hilal kwa mabao 2-0 kisha ikaenda kufungwa tena 2-0 na MC Alger ikiwa ugenini na kama itaendeleza gundu hilo, itakuwa katika nafasi finyu ya kurejea historia ya msimu uliopita ilipovuka hadi robo fainali.

Attachments