Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuujulisha umma kuwa usaili wa Walimu Daraja la IIIC – Kiswahili uliopangwa kufanyika tarehe 28 Januari, 2025 katika vituo mbalimbali nchini, sasa utafanyika tarehe 30 Januari, 2025 kuanzia saa 1.00 Asubuhi.
Mabadiliko haya yametokana na uwepo wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati utakaofanyika Jijini Dar es Salaam, uliosababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara tarehe 27 na 28 Januari, 2024. Hali hii inaweza kusababisha changamoto ya usafiri kwa wasailiwa wanaotoka katika Jiji hilo na hivyo kushindwa kufika katika vituo vyao vya usaili kwa wakati.
Tarehe nyingine za usaili, mahali pa kufanyia usaili na muda wa usaili utabaki kama ulivyo kwenye matangazo ya awali ya kuitwa kwenye usaili.