Utaratibu wa kupata Internship taasisi X (ya serikali) kupitia TAESA? Maombi yangu hayajapata mrejesho.

Utaratibu wa kupata Internship taasisi X (ya serikali) kupitia TAESA? Maombi yangu hayajapata mrejesho.

Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita TUNDURU SECONDARY SCHOOL 2026-S0404 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Katika Mtihani wa Form six (ACSEE) 2026/2027 jumla ya wanafunzi wengi wamefaulu.
Bonyeza hapo juu kujiunge na Group la wanachuo waliomaliza kidato cha sita 2026 hapa baada ya matokeo ya form six 2026

JB2025

New member

Joined
Sep 30, 2025
Messages
1
Habari wanajukwaa,

Naomba msaada wa ufafanuzi au uzoefu kwa yeyote aliyewahi kupitia utaratibu wa kuomba nafasi ya internship kwenye Taasisi X ( ya Serikali) kupitia TAESA.

Niliwasiliana na Taasisi X kuhusiana na nafasi za internship, lakini walieleza kuwa wao hawapokei maombi moja kwa moja, bali wanapokea kupitia TaESA. Hivyo walinishauri nitume maombi kupitia taasisi hiyo


Tangu nifanye hivyo, sijapata mrejesho wowote kutoka TAESA licha ya kufuatilia kwa muda sasa kupitia mawasiliano mbalimbali, ikiwemo kutuma barua pepe na ujumbe wa WhatsApp kwa wahusika waliotajwa.

Maswali yangu:

1. Je, ni utaratibu wa kawaida kuchelewa kupata mrejesho kutoka TAESA?

2. Kuna anayefahamu njia mbadala au hatua ya kuchukua ili kufanikisha zoezi hili?

3. Ikiwa Taasisi X hawajasema moja kwa moja kuwa nafasi ipo, je bado ni sahihi kuendelea kusubiri kupitia TAESA?

Naomba msaada wenu kwa yeyote aliye na taarifa sahihi au aliyepitia hali kama hii.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom