Wasailiwa wa kada zote zilizopangiwa kufanya usaili wa mahojiano tarehe 7 Disemba 2024 katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mnajulishwa kuwa kuna mabadiliko ya tarehe ya kufanya usaili huo. Usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 6 Disemba 2024 badala ya tarehe iliyotangazwa awali. Aidha mahali na muda wa kufanya usaili utabaki kama ulivyo kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya www.ajira.go.tz